×

Exclusive: Darassa Afunguka Yote / Hakuna wa Kunifunika, Madawa Mmh” – VIDEO

MKALI wa muziki wa Hip Hop Bongo, Darrasa CMG, amepiga stori na Global TV kuhusiana na kilichomfanya akakaa kimya kwa muda mrefu sana kabla ya siku za hivi karibuni kuachia ngoma yake mpya ya Achia Njia.

Darasa ambaye kimya chake kilizua gumzo sana mitandaoni huku kikiandamwa na maneno mengi kuwa anatumia madawa ya kulevya ndio maana amepoteza dira kwenye muziki amesema maneno hayo hayajawahi kumuumiza kwa sababu alijua mashabiki wake wanampenda sana na wamemmisi ndio maana wanamlilia arudi.