
KIKOSI cha Coastal Union leo kimelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Coastal Union walianza kufunga bao dakika ya 30 kipindi cha kwanza kupitia kwa mshabuliaji wao Haji Lugando akimalizia pasi aliyopewa na Roben Lyanga aliyefunga kwa kichwa.

Iliwalazimu Yanga kusubiri mpaka dakika ya 76 kupindua meza kwa kusawasisha bao kupitia kwa Deus Kaseke ambaye aliingia dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu kwa kumalizia pasi ya Matheo Athony.

Kwa matokeo hayo Yanga wanaongeza pointi moja na kuendelea kujikita kileleni wakiwa na pointi 54 na Coastal Union wakiongeza pointi moja na kufikia pointi 29 wanabaki nafasi ya saba.

