SOKO LA MASTAA WA KIKE BONGO KUHAMIA DUBAI…SIRI YAFICHUKA!
IMEFICHUKA! Baada ya awali mastaa wengi Bongo kuonekana kukimbilia sana nchini China, Ijumaa Wikienda limebaini kuwa kwa sasa mastaa wengi hususan wa kike, soko lao limehamia nchini Dubai huku siri kadhaa za wanachokifuata zikitajwa.
Mnyetishaji wetu aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa mastaa wetu mara nyingi wamekuwa wakionekana kwenda Dubai ambapo hujiachia na kuonekana kwenye mitandao lakini nyuma ya pazia kuna siri zinazowapeleka.
“Wengi wao wameanzisha biashara ndogondogo za manukato na udi, vitu hivi vinapatikana kiurahisi huku lakini wengine wana soko kubwa la kisanii ndiyo maana wanakuja huku,” alisema sosi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jamila. Aidha, Jamila alidai kuwa hata hivyo pamoja na wao kufanya biashara lakini wapo wanaofika mjini hapo kwa ajili ya kudanga ambapo hukutana na wanaume wenye fedha zao na kuwawezesha.
“Wapo wanaofika huku kwa ajili ya kudanga wanaume wa Kiarabu wanatoa dau kubwa sana kwa wasanii ndiyo maana wakifika huku wanajiachia kwani bata wanalopewa si la nchi hii,” alisema sosi huyo.
Sosi alienda mbali zaidi na kudai kuwa, mbali na hao wanaopenda kwenda kudanga, watu wa Dubai huwa wanawapenda sana wasanii au watu wenye majina hivyo huwapapatikia na kuwaonesha ukarimu hivyo ni rahisi mtu kupata rafiki ambaye ana uwezo wa kumgharamia kwa kila kitu.
Wapo wanaokwenda kwa ajili ya kutumbuiza kwenye sherehe za harusi mbalimbali na sherehe za watu binafsi, lakini wapo wanaopiga shoo kama vile mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’. Baadhi ya mastaa waliofika Dubai na kufunguka yaliyowapeleka ni pamoja na Halima Yahya ‘Davina’ ambaye alisema amekuwa akienda kwa ajili ya biashara yake ya manukato.
Aunt Ezekiel naye amekuwa akienda mara kwa mara Dubai lakini alieleza kuwa mara nyingi huenda kwa ajili ya mapumziko ambapo hivi karibuni alikwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa lakini mpaka sasa (juzi) yupo nchini Dubai akiwa na kundi la mastaa wenzake; Jacqueline Wolper, Vivi pamoja na Davina ambapo wanadaiwa kwenda kwenye sherehe ya kibao kata.
Staa mwingine aliyewahi kwenda Dubai ni pamoja na Irene Uwoya ambaye alikwenda kwa ajili ya mapumziko pamoja na rafiki yake. Mbali na wote Kajala Masanja naye amewahi kwenda Dubai ambapo alikwenda kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Comments are closed.