×

Rais wa Korea Kaskazini Atumia Treni kwenda kukutana na Rais Trump

Kim Jong Un akiwa ndani ya usafiri wa treni kwenda nchini Vietnam.

Idara ya habari ya Ikulu nchini Korea Kaskazini imethibitisha Kiongozi wao, Kim Jong Un anatumia usafiri wa treni kwenda nchini Vietnam kushiriki kikao chake cha pili na Rais wa Marekani, Donald Trump.

 

Shirika la habari la Korea Kaskazini, mapema leo limeripoti kuwa Kiongozi huyo ameambatana na Kim Yong Chol, ambaye ni msaidizi wake muhimu katika majadiliano hayo pamoja na dada yake, Kim Yo Jong.

 

Majadiliano hayo yanayohusu silaha za nyuklia yamepangwa kufanyika Jumatano na Alhamisi wiki ijayo katika mji mkuu wa Vietnam, Hanoi.

 

Katika mazungumzo ya kwanza yaliyofanyika mwezi Juni 2018 nchini Singapore yalimalizika bila kuwa na makubaliano makubwa juu ya Korea Kaskazini kuachana na silaha za nyuklia