WEMA NIMEKAA MIEZI SITA BILA KUFANYA MAPENZI
UNAPOTAJA majina ya wanyange bora ambao wamedumu kwa zaidi ya miaka 10 wakiwa juu basi huwezi kumuweka kando Wema Isaac Sepetu.
Wema ambaye mashabiki zake wanamtambua zaidi kama Madame, ustaa wake umekuwa na mambo na vituko vingi vya hapa na pale.
Ukianza kuhesabu msururu wa wanaume aliotoka nao, ni mrefu mno, lakini hivi sasa anasema hana mtu tangu Septemba, mwaka jana.
Hivi karibuni katika Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) alifanya mahojiano na vyombo vya habari na kujibu maswali mbalimbali kama ifuatavyo.
UNA NYWELE FUPI KWA SASA, JE UTABADILISHA?
“Huu ni mwonekano ambao nimeamua kuwa nao kwa mwaka 2019 mzima, sitabadilisha.
“Labda mkiniona kwenye kazi ndiyo naweza kubadilika lakini hivi mkiniona mimi sitabadilika.
“Ninasikia raha sababu Dar kuna joto.
VIPI MAHUSIANO?
“Niko ‘single’ tangu mwezi wa tisa mwaka jana, tena sija-du na mtu yeyote.
KUNA WANAUME WANAOKUFUATA?
“Wako wengi sana, yaani wengimno, mpaka daaah!
UNAWEZAJE KUKAA SINGLE KWA MUDA WOTE HUO?
“Kuna muda mtu unaona bora upumzike masuala hayo, kama mimi nimechukua muda wa kuwa mwenyewe tu bila ya masuala hayo.
“Ninaweza kujizuia, tena watu ambao wanaonizunguka na kunipenda wananipa furaha.
ULISEMA HUIPENDI INSTAGRAM, KWA NINI?
“Siyo kama siipendi Insta ila sipendi mambo yake ya huko, yaani kama mambo ya umbea. Ninachofanya ninaitumia kama sehemu ya kutangaza biashara zangu.
“Tena kama nikiposti kitu sitaki kuangalia komenti, naenda WhatsApp, ninatafuta vitu vya kunifanya niwe bize. Sipendi umbea.
KWA NINI UNAPENDA KUVAA MAVAZI MEUSI?
“Kwa sababu mavazi haya hayajawahi kumuangusha mtu, kwenye ‘event’ kama hizi huwezi tu kujivalia lazima uvae kama hivi.
VIPI MASULA YA KUWA NA MTOTO?
“Mwenyezi Mungu akinibariki nitamshukuru, nitasema Alhamdulillah.
NINI MIPANGO YA WEMA MWAKA HUU?
“Watu wasubiri kuona kitu gani nitafanya, nina vitu vingi sana kwa mwaka huu lakini siwezi kuvisema kwa sasa.
MWAKA JANA NA HUU KWAKO KUNA TOFAUTI GANI KWENYE FILAMU?
“Nimekaza tu palepale, kila siku nimekuwa nikisema nataka kuwa zaidi ya jana. Unajua naipenda kazi nisiwe muongo naichukulia sana siriazi, nadhani ni hivyo,” anasema Wema.
Makala – Bongo | SAID ALLY
Comments are closed.