BI. Mwanaidi Salehe, mkazi wa Mkoa wa Pwani amemlilia Rais Dkt. John Magufuli amsaidie ili aweze kupata haki yake baada ya kubomolewa nyumba zake nne alizokuwa akiishi katika Kijiji cha Mazingara wilayani Bagamoyo.
Akizungumza na Global TV, ka uchungu huku akimwaga machozi Mwanaisha ambaye kwa sasa amejihifadhi kwa ndugu zake maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam, amemuomba pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi wamsaidie aweze kupata haki yake kwani anateseka.