×

MAKONDA AMPONGEZA MKURUGENZI TEMEKE – VIDEO

MKUU wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda amempongeza Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke, Lusubulo Mwakabibi kwa kusimamia miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa katika wilaya hiyo.

 

Akizungumza na Global Publishers, wakati wa ziara ya kukagua miradi katika wilaya hiyo, Makonda alisema anampongeza Mwakabibi kwa sababu ameridhishwa na ujenzi wa barabara ya Temeke Hospitali kwa kuwa mkandarasi amejenga barabara nzuri kwa gharama nafuu.

“Nampongeza kwa sababu amechagua mkandarasi ambaye amejenga barabara nzuri na kwa gharama nafuu na karibu miradi yote katika wilaya hii imeenda vizuri. Nimeona barabara zote zimejegwa kwa kiwango kizuri.

 

“Pia miradi mingine imeenda vizuri ikiwemo kisima cha maji Charambe pamoja na ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kijichi, ujenzi wa ghorofa mbili Zahanati ya Yombo Vituka pamoja na bweni la wanafunzi wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Tuangoma.

“Ningetamani kama jina la bweni lingeitwa jina la mmoja wa wanakamati ambaye amezikwa jana ambaye nimeambiwa anaitwa Ibrahimu Mketo na ninawapa pole wanakamati kwa kupata msiba huo,” alisema Makonda na kuongeza:

 

“Kikubwa tunatimiza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuona miradi yote inakamilika ili wananchi waweze kupata huduma zinazostahili.”

Stori: Neema Adrian, Dar