
WATU 30 wamekamatwa kwa kuuza, kusafirisha na kutengeneza pombe za kienyeji katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake na kusema watu hao walikamatwa wakiwa na lita 314 za pombe haramu aina ya gongo na kwamba oparesheni hiyo ni juhudi za kutokomeza ulevi wilayani humo.
Wakati huohuo, Hokororo alisema ni marufuku kwa mtu yeyote kunywa pombe nyakati za mchana.
Aidha, amekanusha taarifa zilizosambaa kuwa wilaya hiyo ina aina 52 ya pombe na kusema kuwa zipo aina 11 tu.