×

MAMA KANUMBA: RAY TUNAPISHANA, LULU HATUJAONGEA MIAKA 5 – VIDEO

MAMA wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Bi. Flora Mtegoa,  amefunguka kuhusu uhusiano wake kwa sasa na waliokuwa maafiki wa mwanaye wakiwemo ni Vincent Kigosi ‘Ray’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’.

 

Akizungumza na Global TV Online, mama huyo amesema hana matatizo na wasanii hao licha ya kutowasiliana nao mara kwa mara tangu mwanaye alipofariki dunia Aprili 7, 2012 baada ya kudaiwa kusukumwa na Lulu kisha kuanguka na kufariki dunia.

Aidha, baada ya kulipwa Tsh. Milioni 15 kama kiinuamgongo kutoka kwenye makampuni yaliyokuwa yakifanya kazi na mwanaye,  amesema ameiomba serikali imsaidie kutengeneza documentary (makala) ya marehemu Kanumba.

 

Ameongeza kuwa Kampuni ya Steps Entertainment imekubali kumsaidia kukamilisha makala hiyo lakini pia anawaomba wadau mbalimbali wamsaidie kumchangia ili kukamilisha makala hiyo ya marehemu Kanumba.

 

MSIKIE MAMA KANUMBA HAPA