×

Yanga Princess yapata ahueni

TIMU ya Yanga Princess imepata matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu katika Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite mara baada ya juzi kuichapa Baobab Queens kwa mabao 4-2, Karume, Dar.

 

Yanga Princess ilianza vibaya raundi ya 15 na 16, baada ya kujikuta ikipokea vipigo kwenye michezo hiyo huku kipigo
kikubwa ni kikiwa cha mabao 5-1 dhidi ya Simba Queens.

 

Kwa matokeo iliyoyapata juzi, imefanya ikusanye jumla ya pointi 22, ikisalia katika nafasi ya saba nyuma ya Kigoma Sisterz, walio na pointi 25 kabla ya mchezo wao wa jana.

 

Kocha Msaidizi, Hamisi Kinonda, aliliambia Championi Jumamosi; “Ushindi tuliopata juzi umefufua matumaini yetu ya kumaliza katika nafasi nne za juu na kwa upande fulani umewaongezea wachezaji hali ya kujiamini.”