×

RC Chalamila: Wamefukua Kaburi la Albino, Wameiba Mifupa – Video

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila,  awetaka wananchi wa mkoa huo kutoshiriki vitendo vya kishirikina vinavyosababisha ubakaji, ulawiti na mauaji ya baadhi ya watu kwa kuamini kuwa watapata utajiri wa fedha na mali haraka.

 

Chalamila ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa salamu za mkoa huo kwenye  ziara ya Rais Magufuli, wilayani  Chunya alipokuwa akizindua Barabara ya Chunya-Mbeya na uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa barabara ya Chunya-Makongorosi uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba, mjini Chunya.

 

“Hapa Chunya bado kuna tatizo la ulawiti na kunyanyaswa wanawake na watoto.  Mwezi uliopita kuna mtoto alibakwa na kutumbukizwa kwenye migodi, juzi kuna jamaa alifungwa miaka 30 huko Mwanza, jaji alipohukumu akasema kesi ya ubakaji haina mashiko, aliachiwa akaja Mbeya, akamteka mtoto na kuanza kumpigia simu mzazi wake akiomba shilingi milioni 10 ili amrudishe huyo mtoto.

 

“Bahati mbaya alimuua huyo mtoto, Aprili 9, mwaka huu, jeshi la polisi wakamtia mbaroni wakati akitaka kukimbia, sasa hivi yupo hapo anasubiri kuhukumiwa, juzi pale Rungwe wamefukua kaburi la mtoto aliyezikwa miaka ya nyuma wakaondoka na viungo.  Sasa tunasema jambazi wa aina yoyote tutamshughulikia, tunaambiwa Chunya ndiyo inaongoza kwa kutorosha madini, hii ni aibu sana,” alisema akiziomba mahakama kutoa haki na akatoa tahadhari kwa wananchi kutoshiriki vitendo vya kiovu kupitia ushirikina.

 

VIDEO: MSIKIE CHALAMILA HAPA AKIFUNGUKA

<C/ENTER>