Rais Dkt John Magufuli akizindua hospitali katika Kata ya Mwakibete mkoani Mbeya amewataka watoa huduma za afya kutoa huduma hata kama mtu hatakuwa na fedha, ili apone arejee kulitumikia taifa. Rais anaendelea na ziara ya kikazi mkoani humo.
“Nimekua mkali kwa mafisadi na wala rushwa kwa sababu rushwa ni adui wa haki. Natoa agizo kwa TAMISEMI kuikamilisha Hospitali ya Wilaya ya Mbarali kabla ya mwaka huu kuisha. Nawahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na watoa huduma wengine wakiwemo wa Makanisa, Misikiti na watu binafsi kwa sababu Serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu peke yake.
“Natoa rai kwa Hospitali ya UWATA kutoa huduma bila kuwabagua wananchi kwa dini pia muangalie suala la gharama kwa sababu sio wananchi wote wana uwezo wa kulipia gharama kubwa za afya hasa ukizingatia Serikali pia inachangia.
“Nawaahidi kuijenga barabara hii ya Hospitali ya UWATA yenye mita 700 kwa kiwango cha lami pia naichangia Shule ya Sekondari Mwakibete shilingi mil.5 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 200 ya shule hiyo,” amesema Rais Magufuli.