The House of Favourite Newspapers

Wamwagiwa minoti kuimaliza Yanga SC

LIPULI FC ya mkoani Iringa imejipanga kisawasawa kuhakikisha inawatuliza wapinzani wao, Yanga watakaokutana nao Mei 6, mwaka huu katika mchezo wa Kombe la FA. Lipuli FC inatarajiwa kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Samora Iringa katika hatua ya nusu fainali.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Lipuli FC, Julius Leo alisema wamekuwa wakikusanya fedha kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi pamoja na FA kuhakikisha wachezaji wake hawana matatizo yoyote kuelekea mchezo huo kwa kuwapatia mishahara yao.

 

“Kuna harambee ambayo tumeifanya hivi karibuni lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwapatia wachezaji wetu waweze kumaliza vizuri ligi ikiwa ni pamoja na kushinda mchezo wa FA kuhakikisha tunawalipa mishahara yao kabla ya mchezo huo kufi ka.

 

“Tunahitaji kusonga mbele zaidi kwa kushinda mechi hiyo ili kuweza kutinga hatua ya fainali,” alisema Leo.

Comments are closed.