×

ALBAM YA INDIGO YAWAKUTANISHA CHRIS BROWN, DRAKE

MWANAMUZIKI wa Marekani,  Chris Brown,  ametoa orodha ya majina ya wasanii ambao atawashirikisha kwenye album yake mpya inayokuja  ya ‘’INDIGO’’ ambayo inatarajiwa kutoka mwezi Juni mwaka huu.

Kwenye orodha hii  usishangae kukutana na majina ya wasanii wakubwa kama Justin Bieber, G-Eazy,Nick Minaj, Tory Lanez, Tyga, Lil Jon, H.E.R, na Lil Wayne.  Kubwa zaidi ni pale jina Drake lilipoonekana kwenye orodha hiyo na kufanya mashabiki wake kuwa na hamu kubwa kusikia kolabo baada ya kumaliza bifu lake na Chris Brown lililodumu kwa muda mrefu ambapo huenda hiyo ikawa ni albam bora zaidi mwaka  huu 2019 kwa Chris Brown.