
MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, umewasili katika Ukumbi wa Karimjee, ulioko Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho na kuagwa leo Jumanne, Mei 7, 2019.

Viongozi mbalimbali akiwemo Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu, viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, taasisi, dini na wananchi wamejitokeza kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Mengi.

Nje ya Ukumbi kuna wanafamilia wengi wa Mengi ambao si ndugu zake wa damu, wengine hawajawahi hata kuonana naye lakini aligusa maisha yao.




