
TIMU ya Yanga Princess itavaana na Evergreen kwenye Uwanja wa Karume leo Jumapili.
Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote kwa kuwa kila timu inahitaji pointi tatu ili ikae pazuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Evergreen wapo nafasi ya pili kutoka chini na pointi zao tisa, huku Yanga Princess wapo nafasi ya saba na pointing zao 22.

Nahodha wa Evergreen, Fatuma Issa, (Fetty Densa) amesema wataingia Uwanjani kupambana kufa na kupona ili wapate pointi tatu, zitakazowapa unafuu kwenye msimamo.
“Mechi ni ngumu kweli ila tutaingia kupambana kufa na kupona ili tushinde kwa kuwa hali yetu kwenye msimamo siyo mzuri,” alisema Densa.
Mohammed Mmachinga, kocha wa Yanga Princess, alisema, “mchezo huu ni muhimu kwetu wote kwa kuwa tunahitaji pointi tatu ili tukae sawa kwenye msimamo.”
