×

GIGY ACHOMOA BIFU NA MO J

MSANII wa kizazi kipya, Gifty Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa hana bifu lolote na mzazi mwenzake Mourad Alpha ‘Mo j’ kwa sababu kila mtu sasa hivi ana maisha yake, hivyo hakuna wa kumuingilia mwenzake.

 

Akizungumza na SHUSHA PUMZI, Gigy alisema ni muda mrefu umepita tangu aachane na mwanaume huyo, na huko aliko anafuraha zaidi kwani anapata kila anachokipata, pia anamshukuru Mungu mzazi mwenzake huyo anamlea mtoto wao Mayra bila shida yoyote.

 

“ Unajua sasa hivi nina furaha sana kwenye haya mahusiano yangu mapya, huyu kaka ananipenda jamani sijawahi ona, huwezi amini nimeridhika kwa sababu napata kila ninachokitaka, pia nashukuru Mungu zilipendwa wangu (mzazi mwenzake) licha ya kutengana kwetu lakini bado anampenda na kumjali sana binti yetu Mayra, hivyo siwezi kuwa na bifu naye kwa sababu anamtunza mwanetu,” alisema mrembo huyo.

 

STORI: Memorise Richard