Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ambaye pia ni balozi wa Danube Home, leo Mei 25, ametembelea duka la Danube lililopo Mlimani City na kufanya shopping ya nguvu.
Wakati akiendelea na shopping hiyo, Diamond, akaamua kumnunulia zawadi shabiki yake mmoja ambapo bahati ikaangukia kwa Mama mmoja anayeitwa Wema, mkazi wa Shekilango, ambaye amepiga stori na Global TV na kuelezea furaha yake baada ya kupokea zawadi hiyo