Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaahidi wachezaji wa Klabu ya Simba waliojishindia Tuzo za Mo Simba Awards usiku wa kuamkia leo waoongozwa na Golikipa wao namba moja, Aishi Manula, kufika ofisini kwake Jumatatu ya Mei 03, kwa ajili ya kuchukua zawadi yao ya Tsh milioni 1 kwa kila mchezaji na Golikipa huyo atapewa Tsh milioni 10.
MO SIMBA AWARDS 2019
Tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka – Aishi Manula.
Tuzo ya Beki Bora wa Mwaka – Erasto Nyoni akiwapiku Shomari Kapombe na Pascal Wawa.
Tuzo ya Kiungo Bora wa Mwaka – James Kotei akiwapiku Jonas Mkude na Mzamiru Yasin.
Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka – John Bocco akiwashinda Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.
Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo – Rashid Juma akiwapiku Adam Salamba na Paul Bukaba.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike – Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’.
Tuzo ya Wachezaji – Erasto Nyoni (Chaguo la Wachezaji wenzake).
Tuzo ya Mfungaji Bora (Kiatu cha Dhahabu) – Meddie Kagere ambaye pia ndiye mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliomalizika akiwa amefunga magoli 23.
Tuzo ya Heshima – Hazim Dewji.
Tuzo ya goli bora la msimu – Clatous Chama alilofungwa dhidi ya Nkana FC kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka – Meddie Kagere.