×

BETIKA HALINA MPINZANI MTAANI


WASOMAJI wa Gazeti la Betika mitaa ya Mwanyamala na Kinondoni Mkwajuni, wamesema kuwa gazeti hilo limeendelea kuwa msaada mkubwa kwao katika ishu za kubeti.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, limekuwa likitolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 ambapo lina kurasa 20 ambazo zote ni za rangi.

Gazeti hilo linaloingia mtaani kila Jumatano, leo timu ya Maofisa Masoko ya Global Publishers ilitembelea Mwananyamala na Kinondoni Mkwajuni jijini Dar na kukutana na wasomaji kadhaa waliotoa maoni yao juu ya gazeti hilo.

“Tumefurahi sana leo kututembelea huku kwetu, nadhani hii ni mara ya kwanza mnafika maeneo haya, tunawakaribisha sana lakini hili gazeti tumekuwa tukilipata kila linapotoka tangu hapo awali.

“Tunawapongeza kwa kulileta gazeti hili lenye makala na uchambuzi mbalimbali wa mechi ambao unatusaidia katika kubeti, kwa sasa halina mpinzani,” alisema Ally Juma ambaye ni mmoja wa wasomaji hodari wa Gazeti la Betika.

Kwa upande wa Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisisitiza kwamba, lengo kubwa la Betika ni kumfikia kila Mtanzania katika pande zote za nchi na wao kama timu, watahakikisha wanafika popote pale kwenye makazi ya watu.

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

“Tumejipanga kuhakikisha tunafika kila sehemu ambapo kuna makazi ya watu, kubwa zaidi ni kuwafikishia hili gazeti ambalo lina maujanja mengi ya kubeti, hivyo nyie wakazi wa Kibaha endeleeni kulipokea vizuri gazeti letu.

“Pia bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu, tunawakaribisha ofisini kwetu Sinza Mori jijini Dar,” alisema Mgema.