MSANII wa filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amejikuta katika wakati mgumu na kupata kiwewe wakati akisubiri majibu ya Ukimwi muda mfupi kabla ya kujitolea damu katika wiki ya damu salama duniani iliyofanyika hivi karibuni.
Zoezi hilo la uchangiaji damu lilifanyika wiki iliyopita ambapo Davina na wasanii wenzake wanaounda Chama cha Wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini (CWFT) walikuwa na zoezi la uchangiaji damu lakini shida ilikuwa kwenye kupimwa afya kabla ya kujitolea damu hiyo.
Akizungumza na paparazi wetu Davina alisema zoezi hilo lilifanyika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ambapo walialikwa kwa ajili ya zoezi hilo.
“Kabla hatujatoa damu tulipima Ukimwi, kifua kikuu na maradhi mengine yaani nilikuwa na kiwewe na wasiwasi mkubwa sana lakini namshukuru Mungu baada ya kupimwa maradhi yote hayo nilibainika kuwa niko fiti hapo ndipo niliposhusha presha ingawa hata hivyo hiyo haikuwa mara yangu ya kwanza kuchangia damu,” alisema Davina.