×
Global Publishers
  • Home
  • Habari
    • Kimataifa
    • Kitaifa
  • Global TV
  • Magazeti
  • Ajira
  • Burudani
    • Audio Music
    • Music Videos
    • Dar Live
  • Michezo
  • Makala
    • Afya
    • Mahaba & Maisha
    • Burudani
    • Hadithi
    • Mikasa
    • Siasa
  1. Home
  2. Habari
  3. M-pawa kuongeza faida mara mbili wateja wake kwa kuwazawadia washindi wa droo ya 3

M-pawa kuongeza faida mara mbili wateja wake kwa kuwazawadia washindi wa droo ya 3

Global Publishers June 27, 2019
SHARE THIS:
CBA na Vodacom wametangaza leo washindi wa droo ya 3, kwa ajili ya promosheni yao ya kuadhimisha miaka 5 ya huduma ya Mpawa yenye lengo la kuwahusisha kifedha wateja wake kwa kuwazawadia. Promosheni hii ilifanyika katika makao makuu ya benki hiyo  jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washindi wa dro ya M-PAWA namba 1, 2 na 3 ni Mangu Zanura, Nyerenga Rahim, Robert Tuisenge, Mwafumba Martha, Ayilla Agness, Kayombo Hilda, Mollel Charity, Gwandu Elizabeth, Agust Emannuel, Tezeyo Abinal, Mwita Joseph, Haule Reginberti, na Kabona Fadhili, pamoja na wengine wengi waliotangazwa mbele ya mwakilishi wa bodi ya michezo Bi Chiku Salehe na wawakilishi wa benki ya CBA.
Watumiaji wa M-Pawa wamepanda kwa kasi kufikia millioni 8.5 tangu izinduliwe,huku wengi wa wateja hao wakiwa wafanya biashara wanawake, vijana na mamillioni ya Wa-tanzania, hasa maeneo ya vijijini ambapo huduma za benki ni za kiwango kidogo kwasababu ya ukosefu wa taasisi za benki au upungufu wa mahitaji ya kifedha.
“Kampeni hii ya Miaka 5 ya Mpawa imelenga kudumu kwa wiki 6 na leo ikiwa ni droo ya 3, tumekua na zaidi ya washindi 1000 mpaka sasa tangu ilipoanza, ambapo baadhi ya washindi wameondoka na mara mbili ya akiba ya kuanzia na shilling 1000 mpaka 200,000 za Kitanzania, simu za kisasa, vocha pamoja na zawadi nyingine huku washindi wengine wakiongezeka kwenye droo zilizobaki.” Aliongea Bi. Maria Marbella, Mwakilishi kutoka benki ya CBA, aliongeza kwa kusema kuwa mshindi wa kwanza wa promosheni hii atazawadiwa millioni 15 ya kitanzania kwenye droo ya mwisho hivyo tunaendelea kuwasisitiza watumiaji wa Mpawa kuweka akiba na kurejesha mikopo mapema ili waweze kupata nafasi ya kushinda.
“Mpawa ni huduma iliyoleta mapinduzi ya kibenki ambayo inaruhusu watumiaji wetu kuweka akiba kwa njia ya simu, na kupata faida kutoka kwenye akiba yao na hatimaye kuongeza kiwango cha mikopo yao. Kutumia njia hii tunawawezesha wateja wetu kuendeleza mitaji yao kwa ajili ya baadae na kufikia baadhi ya ndoto zao. Kwahiyo basi tunawapongeza washindi wa 3 wa droo pamoja na washindi wetu wote waliopita. Inatupa faraja kubwa kuwazawadia wateja wetu waaminifu na tunafurahia kuona wananufaika kutokana na huduma zetu” aliongezea Bi Maria Marbella, Mwakilishi wa Benki ya CBA.
Ili kushiriki na kushinda kwenye droo hii, mteja wa MPAWA anatakiwa kuweka akiba isiyopungua kiasi cha Tsh 1000 za kitanzania, kukopa na kurudisha mapema mkopo wake na hapo papo atakuwa ameingia kwenye droo na kujiwekea nafasi ya kushinda.
SHARE THIS:
Previous Next

Related Posts

Mchekeshaji Maarufu Wa Tiktok Atembelea Kwao Senegal, Alamba Dili Na UNICEF – Video - Global Publishers HABARI

Mchekeshaji Maarufu Wa Tiktok Atembelea Kwao Senegal, Alamba Dili Na UNICEF – Video

February 3, 2025
Charles Matondane Ateuliwa Kuwa Meneja Mpya Wa Bolt Nchini Tanzania - Global Publishers HABARI

Charles Matondane Ateuliwa Kuwa Meneja Mpya Wa Bolt Nchini Tanzania

June 18, 2023
Inspekta Haroun: Ustaa, Ujana Vilinitesa - Global Publishers BURUDANI

Inspekta Haroun: Ustaa, Ujana Vilinitesa

July 26, 2017
NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha, Yajadili Fursa, Ufanisi wa Huduma Zake Kwa wateja - Global Publishers HABARI

NBC Yakutana na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha, Yajadili Fursa, Ufanisi wa Huduma Zake Kwa wateja

July 11, 2025


DAKTARI

GLOBAL TV Online




SIMBA
YANGA
NEWS
Global Publishers
  • About Us
Download on the App Store
Get it on Google Play

© 2026 Global Publishers. All Rights Reserved.

Designed by Yatosha Web Services