×

Mfanyabiashara wa Kenya Aliyepotea Tanzania, Mkewe Afunguka Mazito

MKE wa mfanyabiashara maarufu wa Kenya na msaidizi wa Mbunge Zitto Kabwe, Raphael Ongangi,  ameendelea kupaza sauti akiomba msaada kwa mtu yeyote kusaidia alipo mume wake huyo ambaye aliripotiwa kuchukuliwa na watu wenye silaha tangu Jumatatu wiki hii jijini Dar es Salaam na hajulikani alipo.

 

Veronica Kundya ambaye ni mke wa Ongangi ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram: “NAKUSHUKURU SANA KWA MAOMBI ILA PIA KWA KUSHARE NA WATU WENGI ZAIDI UWEZAVYO 🙏🙏🙏 ni ngumu kuelewa ila hata kwa asilimia ndogo tu naomba please put yourself into the shoes of RAPHAEL, my shoes as his wife and his kids and the shoes of Raphael’s very close people 😭😭😭😭😭😭”

“Na mnisaidie KUMWITA MUNGU ZAIDI HATA KIFUPI na sio kwa maneno tu kwamba tupo pamoja ktk maombi ila fanya kweli hata kwa dakika moja tu sema MUOMBE MUNGU AWE NA RAPHAEL NA SISI WOTE INCLUDING WEWE NA FAMILIA YAKO 🙏🙏🙏”

“Mana tunahitaji sana TAARIFA KUSAMBAA KWA UMMA , tupate msaada zaidi hivo NAOMBA NAOMBA UTUSAIDIE KUSHARE HII TAARIFA KWA KASI NA BILA KUCHOKA, SHARE kwa friends and relatives , groups zote ulizopo , social media , influencers wote unaowajua , your close people with authority , ili kila mtu aweze kufahamu na kuongeza macho ya kuangaza ili iwe rahisi zaidi kunotice chochote kitakachosaidia kupatikana kwake.”

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jana lilisema:  “Hatuna uthibitisho kwa suala la utekaji sababu ni jambo linalofanyiwa uchunguzi lakini sababu ni taarifa tumezipata kutoka kwa Mke wake jitihada za kumtafuta Mtekaji zinafanyika kwa juhudi sana, tuna imani tunaweza kufanikiwa sababu tayari Watu wamejaa mitaani kwa ajili ya kuendelea kuhangaika tukishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.”