×

Makonda azuia Yondani, Nyoni kustaafu Stars

MWENYEKITI wa Hamasa wa Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon, Paul Makonda amesitisha mipango ya wachezaji wakongwe Kelvin Yondani na Erasto Nyoni kustaafu kuichezea timu hiyo.

 

Hiyo, ikiwa ni saa chache mara baada ya wachezaji hao kutangaza kustaafu kuichezea Stars wakiwa nchini Misri baada ya timu hiyo kuondolewa hatua ya makundi ya Afcon.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo, Serena Hotel jijini Dar es Salaam mara baada ya kutua nchini, Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar alisema kuwa Yondani na Nyoni bado ni wachezaji wa Stars na hakuna mchezaji yeyote atakayestaafu kuichezea timu hiyo.

 

Makonda alisema, kama Kocha Mkuu Mnigeria, Emmanuel Amunike akiwahitaji kwenye kikosi chake, basi ni lazima wote waripoti kambini kama ilivyokuwa zamani.

 

“Mnatakiwa kufahamu kuwa nyie bado mnahitajika katika timu, hivyo basi Yondani na Nyoni mnatakiwa mlifahamu hilo, tumekuwa kama familia hivi sasa baada ya kuwa pamoja Misri kwenye Afcon,” alisema Makonda.

 

Aidha, Makonda alimuita Yondani na kumpa nafasi ya kuzungumza ambapo alisema: “Nimesitisha mpango wangu wangu wa kustaafu Stars, nitaendelea kuichezea timu yangu.” Upande wa Nyoni alisema: “Nimebaki na nimesitisha mpango wa kustaafu nitaendelea kuitumikia Stars.”

Kocha ZAHERA AWAKA Kuhusu GADIEL MICHAEL – “Mnambembeleza Nini?”