
Mfanyabiashara na staa wa mitandaoni, Junaither Pemba @junaithar ambaye ni dada wa mfanyabiashara maarufu Jack Pemba, amefunguka kuwa hakuwahi kuweka uadui na aliyekuwa mumewe kwani tayari wana mtoto hivyo kuna kipindi anamuhitaji kama baba.

Akizungumza na Global TV, Junaither ambaye alikuwa kivutio kikubwa kwa watu mbalimbali mitandaoni jinsi alivyokuwa akiishi na mumewe huyo, amesema kwa sasa amesha-move on na anamaisha ake mengine.