The House of Favourite Newspapers

FAHAMU KANSA YA TITI, UZAZI, KISUKARI YANAVYOKUWA YAKURITHI

Kuna aina fulani ya magonjwa ambayo hupatikana katika familia,  mengine yanayotokana na kurithi na mengine kwa sababu familia hushiriki mazingira yale yale, mahali wanapoishi, aina ya chakula n.k. Magonjwa ambayo mtu huweza kurithi ni haya yafuatayo.

 

Saratani ya matiti: Kuna jeni (Genes) mbili ‘Breast Cancer Gene 1’ na ‘Breast Cancer Gene 2’ ambayo inaweza kupitishwa katika familia kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine. Iwapo mojawapo wa familia yenu, hasa mama, dada au binti amewahi kuugua saratani ya matiti, kuna muhimu hata nawe ufanyiwe ukaguzi na uchunguzi wa kila mara wa matiti yako.

 

Saratani ya uzazi wa kike (Cervical): Huweza kusababishwa  jeni (genes) kutoka kwa matiti zilizoathiriwa na saratani ya matiti. Iwapo, mama yako, dada au bintiyo amewahi kushikwa na saratani ya uzazi, uko kwenye hatari ya kuupata kwa asilimia 5 katika maisha yako.

 

Ni muhimu uangaliwe na ukaguliwe chembechembe za seli za sehemu za uzazi (papsmears) ili ugunduliwe mapema iwapo una huu ugonjwa na kupewa tiba.

Shinikizo la juu la damu mwilini: Hali hii inaweza kudhibitiwamacho (Glaucoma): Iwapo katika familia yako kuna historia ya Glaucoma, kuna uwezekano mkubwa wewe kuupata ugonjwa huu kwa sababu una uhusiano wa mzazi.

 

Mfadhaiko (Depression): Hii hali hufuata historia ya familia na inaweza kurithiwa. Hata hivyo, si lazima mtu arithi, unaweza kujitokeza tu hata bila mtu yeyote katika familia kuwahi kuwa nao.

Ugonjwa wa kusahau: (Alzheimers) Kuna uwezekano wa mtu kushikwa na Alzheimers iwapo wazazi wake au ndugu wamewahi kuwa nao.

 

Allergy (Mzio) na Asthma: Iwapo mtu ana shida ya mzio kuna uwezekano wa asilimia 50 kuwa mtoto wake atakuwa na shida hii. Iwapo wazazi wote wawili wana mzio kuna uwezekano wa  asilimia 75 kuwa mtoto wao atakuwa nayo. Ugonjwa wa pumu (Asthma) mara nyingi unasababishwa na mzio na watoto wengi walio na asthma pia wana mzio.

 

Ugonjwa wa aina ya FAMM yaani Familial Atypical Multiple Mole Melanoma. Iwapo mtu yeyote katika familia yenu amewahi kuwa na aina hii ya saratani ni muhimu uangaliwe kila baada ya miezi minne au sita. Iwapo una kiuvimbe ambacho kinabadilika na kuwa na uchungu na kuvimba, nenda hospitalini kichunguzwe mara moja.

Kolestroli ya juu (High Cholesterol):

Unaweza kudhibiti hali hii kupitia ulaji wa lishe bora iwapo unaye mzazi ambaye amewahi kupata ugonjwa wa moyo kabla hajafikia umri wa miaka 55, kuna uwezekano kuwa unaweza kupata ugonjwa huu. Hakikisha kuwa unapimwa kila mara.

 

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes):

Aina ya 1 na 2 zinaweza kurithishwa katika familia. Hivyo basi iwapo mojawapo ya watu wa familia yako amewahi kuugua aina yoyote ile ya kisukari ni muhimu kiwango cha sukari mwilini mwako kikaguliwe kila mara kiwe kinachunguzwa. Jambo la kuhuzunisha ni kwamba aina ya 1 haiwezi kuzuilika. Lakini ya pili inaweza iwapo mtu atafanya mazoezi na kula lishe bora kila siku.

 

 

Kansa au  Uvimbe wa ngozi (Malignant Melanoma): Hii ndiyo kansa hatari sana ya ngozi. Kiwaa cheusi (mole) hubadilika na kuwa uvimbe.

 

USHAURI

Yeyote mwenye magonjwa hayo anashauriwa kuonana na daktari wake ili ampime kisha kumpa dawa sahihi za kumtibu ugonjwa husika na ushauri kuhusu tatizo lake.

 

Hata hivyo, watu wengi huwa hawatambui kuwa wana huu ugonjwa hadi wakati ambapo wamechelewa mno. Iwapo una wazazi ambao wana hali hii, ni muhimu ukaguliwe kila mara ili upate matibabu mapema.

Comments are closed.