×

Mimi Mars: Mahusiano ya Vanessa na Jux Yamenipa Funzo (Picha + Video)

Msanii wa Bongo Fleva, Mimi Mars,  akifanya mahojiano na +255 Global Radio Julai 24, 2019.

MSANII wa kike anayefanya vizuri kwenye Bongo Fleva, Mimi Mars, Jumatano, Julai 24, 2019,  amefanya mahojiano na kipindi cha BONGO 255 kinachoruka hewani kupitia + 255 Global Radio iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

 

Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa Mdee amezungumza mengi kuhusiana na kazi zake za muziki, maisha yake na mipango yake ya mbele katika tasnia nzima ya Bongofleva.

Ukiachana na stori za maisha yake na kazi zake ambazo zinafanya vizuri nchini na nje ya mipaka ya Tanzania, amegusia pia kuhusu sakata la filamu ya The Lion King ambayo imezua gumzo  Afrika Mashariki hasa baada ya wasanii wa Afrika Mashariki kutokushirikishwa katika filamu hiyo.

 

Mimi Mars amesema “Sitoiangalia filamu hiyo ikitoka kwa sababu wameni-disappoint sana. Haiwezekani filamu iwe na maudhui ya Afrika Mashariki halafu ukachukue wasanii wa Nigeria…”

Mimi Mars akiwa katika pozi na watangazaji wa Kipindi cha Bongo 255 ambao kutoka kushoto ni Stewart George, Rashid Begani na Sechelela Mazanda (kulia).

 

Kuhusu mahusiano ya Vanessa na Jux kuvunjika, Mimi amesema kuwa mahusiano hayo ya dada yake yamempa funzo kubwa, na kusema kuwa hatokaa awe na mahusiano na mtu maarufu, kwa sababu ameona ‘tension’ iliyokuwepo kwenye mahusiano ya dada yake na kuongeza kuwa mahusiano yake hatoyaweka hadharani.

 

Pia amefunguka kuhusu kumzimia sana msanii Mr. Blue na kuongeza kuwa alianza kumpenda Blue kitambo sana na anatamani sana kufanya naye kazi hata moja.

Tazama Video ya Interview nzima Hapa chini

Mwandishi wa magazeti ya michezo, Martha Mboma (kushoto) akimkabidhi Mimi Mars Gazeti la Spoti Xtra.
Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Rucy Mgina,  akimkabidhi Gazeti la Championi Jumamosi.
Mhariri wa Gazeti la Risasi, Joseph Shalua akimkabidhi gazeti hilo. 
Akiwa na Meneja wa +255 Global Radio, Bori Mbaraka.