
NAHODHA msaidizi wa Taifa Stars, Juma Kaseja amesema kuwa ana imani watafuzu kwenye michuano ya
Chan kutokana na maandalizi wanayoyafanya.
“Watanzania wanahitaji matokeo hilo tunalijua nasi tunapambana kufanya vema kwenye mchezo wetu dhidi ya Kenya.
“Nafasi ni kubwa kwa timu yetu kufuzu michuano ya Chankikubwa ni sapoti na kushirikiana kwani wachezaji tunafanya kazi kwa kushirikiana hivyo na mashabiki watupe sapoti,” alisema Kaseja ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na Simba.
Mara ya mwisho Kaseja aliyewahi kuichezea Moro United, kuitwa Stars ilikuwa ni mwaka 2013.