×

TRA Yaamua Magari Haya Wapewe Wananchi – Video

KILA Jumamosi, ndinga mpya za bei chee zinaanikwa! Kampuni ya Udalali ya Tambaza Auction Mart and General Brockers Ltd iliyopewa idhini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kupiga mnada mali zilizotelekzwa bandarini na zile ambazo wateja wake wameshindwa kuzilipia kodi.

 

Wiki hii tambaza watakuwa na mnada mwingine mkubwa wa hadhara ukihusisha magari na vitu vingine kibao, utakaofanyika katika Bandari Kavu ya Dar es Salaam, Jumamosi hii, Agosti 30, 2019.

Magari hayo ni yale yaliyoingizwa nchini kisha wenye nayo wakashindwa kuyalipia kodi hivyo yakataifishwa na Serikali kwa mujibu wa sheria hivyo yanauzwa katika mnada wa wazi baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.

Akizungumza na Global TV Online, Ofisa wa Tambaza Auction Mart, Sabrina Hamza amesema wananchi wote wanaruhusiwa kwenda kukagua bidhaa zote zitakazouzwa kwenye LCDs zilizopo ofisi za LW9, Bandarini, nyuma ya Police Central kuanzia kuanzia kesho Alhamisi ili siku ya mnada wanunue kirahisi.

(Kwa Mawasiliano piga 0713 327 989 au 0715 683 777 au 0713 508 158 au nenda ofisini kwao, Sinza Mori ama jengo la RITA, Ghorofa ya 18, Posta Dar).

 

TAZAMA VIDEO HAPA