MWANAMKE mmoja nchini Australia amewafungulia mashitaka mahakamani majirani zake kwa kuchoma nyama.
Mwanamke huyo Cilla Careden kutoka jijini Perth, amedai kuwa shughuli za majirani zake za uchomaji nyama, uvutaji wa sigara na kelele za watoto zinavunja sheria za makazi ya watu.

Hata hivyo, mahakama imetupilia mbali madai hayo kwa kusema kuwa hayana maana na hayana ushahidi wa kutosha.
Runinga ya 9 News nchinihumo ilimnukuu Carden akisema: ”Siwezi kufurahi kuona sehemu yangu ya kupumzika majirani zangu wameweka jiko la kuchomea nyama ili harufu inifikie, kani harufu ninayoipenda nia ya samaki tu.”

Bi Carden alikata rufaa ya uamuzi huo katika mahakama kuu nchini Australia ambapo alikabidhi kurasa zaidi ya 400 zenye malalamiko.
Julai 3 mwaka huu mahakama ilisema malalamiko ya mwanamke huyo yamekuwa mzigo mzito kwa majirani ambapo Carden amesema kuwa atachukua hatua zaidi katika mahakama nyingine.