
Jamhuri imemuwekea pingamizi Mkulima Patrick Dezydelius Mgoya aliyefungua kesi ya Kikatiba inayohoji ukomo wa kipindi cha Urais wa Tanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi ameweka pingamizi la awali akiiomba Mahakama iitupilie mbali kesi hiyo bila hata kuisikiliza.
Mgoya amefungua kesi hiyo Mahakama Kuu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiiomba Mahakama itoe tafsiri sahihi ya ibara ya Katiba inayoweka ukomo wa Urais.
Aidha, Mgoya amesema angetamani sheria ya kuweka ukomo wa Rais ndani ya Katiba iondolewe na ukomo wa Rais utokane na sanduku la kura ili Mgombea aweze kuondolewa baada ya miaka mitano au ikionekana anafaa baada ya miaka hiyo basi kura ndio ziamue aendelee.
Kesi hiyo ilitajwa mara ya kwanza jana mbele ya Majaji watatu wanaoongozwa na Jaji Kiongozi, Dkt. Eliezer Felesh Majaji wengine ni Dkt. Benhajj Masoud na Seif Kulita