The House of Favourite Newspapers

MAKONDA KUWAWEKA KIKAANGONI WATENDAJI WALIOKWAMISHA MIRADI

Baadhi ya wakuu wa shule na walimu wakifuatili kwa makini kilichokuwa kikiendelea kwenye hafla fupi ya kukabidhi vyeti na zawadi mbalimbali kwa shule zilizofanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa.
Sehemu walipokuwa wamekaa baadhi ya wakuu wa shule za jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza jambo wakati alipokutana na walimu na wanafunzi wao wakati akiwatunuku vyeti na zawadi mbalimbali.
… Paul Makonda akionesha msisitizo wa jambo mbele ya wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na walimu.
… Makonda akiwatunuku vyeti wakuu wa shule zilizofanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa.
…Wakiendelea kupokea vyeti vya ushindi.
Mmoja wa wakuu wa shule akionyesha cheti alichokipokea kutokana na ushindi wa shule yao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam Mhe. Paul Makonda amehitisha kikao baina yake na watendaji wa Mkoa huo wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Mamea, Wakurugenzi wa Manispaa, Makatibu tawala na wakuu wa Idara ili wamueleze ni kitu gani kinachowafanya miradi ya kimkakati ikiwemo Machinjio ya Vingunguti na Ufukwe wa Coco imechelewa kutekelezwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa fedha za miradi hiyo lakini fedha hizo zimeishia kukaa kwenye Akaunti pasipo utekelezaji.
RC Makonda amesema katika mkutano huo utakaofanyika Jumatano ya September 25 Ukumbi wa Karimjee mtendaji atakaebainika kusababisha uzembe huo atawajibishwa  hapohapo kwa mujibu wa sheria na wengine watazuiwa mishahara yao.
Aidha RC Makonda ametoa wito kwa Wizara ya Utumishi na TAMISEMI kutafuta njia bora ya kuwapata wakuu wa Idara wenye uwezo wa kuleta matokeo Chanya tofauti na sasa ambapo wengi wao wamepanda na kuwa wakuu wa idara kwa kigezo cha kukaa kazini Muda mrefu.
Hayo yote yamejiri leo wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika taaluma na Michezo.

Comments are closed.