×

Mwanajeshi Akamatwa Akitoa Mafunzo ya Kutengeneza Bomu

FBI nchini Marekani limemkamata mmwanajeshi mmoja kwa kutuhumiwa kusambaza taarifa za kutengeneza mabomu kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanajeshi huyo Jarrett William Smith mwenye umri wa mika 24 aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii “Tunaweza kutengeneza mabomu ya simu kama yanayotumika Afghanistan. Ninaweza kuwafundisha hilo.” Aliandika kwenye ukurasa wa facebook

FBI walifanya uchunguzi mweizi Agosti na Septemba mwaka jana na waliweza kupata taarifa za mwanajeshi huyo kwenye ukurasa wake wa Telegram akiwa anazungumza jinsi ya kutengeneza mabomu makubwa ya magari ili kushambulia makao makuu ya vituo vya habari nchini Marekani.

Kwa mujibu wa waendesha mshtaka, Jarrett William Smith amekiri kutoa taariza kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusu namna ya kuunda mabomu alisema kuwa alitoa mafunzo hayo ili ‘azushe ghasia’.

Jarrett William Smith anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 gerezani endapo atapatikana na hatia.