Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchungizi, Erick Kabendera imeahirishwa hadi Oktoba 11, 2019 itakapotajwa tena. Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi bado haujakamilika katika maeneo kadhaa.