DAWA ZA KULEVYA ZILIVYOTEKETEZWA LAIVU!
MAMLAKA ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini (DCEA) jana Oktoba 8, 2019, kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Mahakama, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa , Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), imefanya uteketezaji wa dawa za kulevya ambazo kesi zake zimeshahukumiwa. Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Kamishna Jenerali James William Kaji, amesema dawa hizo ni heroini na kokeni ambazo jumla yake ni kilo 120.91. Uteketezaji huo umefanyika katika kiwanda cha saruji cha Wazo Hill jijini Dar.
Akitoa rai katika uteketezaji huo, Kaji amesema kwa serikali ya sasa inayoongozwa na John Magufuli wale wote waliokuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu waiache mara moja kwani hakuna atakayebaki salama kama ataendelea kuifanya.
Wanahabari waliokusanyika wakati wa uteketezwaji huo walikuwa ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo la kihistoria.
Matukio katika picha:
PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
Comments are closed.