The House of Favourite Newspapers

Ngoma, Chirwa Wakabidhiwa Kuiua Simba

KOCHA msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wamepanga kuwatumia washambuliaji wao Donald Ngoma na Obrey Chirwa katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba kwa kuwa wanaamini watawapa ushindi.

 

Simba na Azam wanatarajiwa kuvaana Oktoba 23 mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wachezaji hao awali walishindwa kuonyesha kiwango kizuri kutokana na majeraha ya mara kwa mara, lakini kwa sasa mambo yanaanza kuwa mazuri kutokana na wote kuwa fiti na kufanya vizuri wakicheza pamoja.

 

Cheche ameliambia Championi Jumatano, kuwa mara nyingi wachezaji hao hupona mmoja na mwingine anakuwa majeruhi lakini kwa sasa wote ni wazima na wameonyesha viwango vizuri hivyo watawasaidia katika michezo yao ijayo ya ligi husasani unaofuata dhidi ya Simba.

 

”Ngoma na Chirwa tunatamani kuwatumia wote kwa pamoja katika safu ya ushambuliaji lakini mara nyingi mmoja akiwa mzima mwingine anakuwa majeruhi, lakini kwa sasa wote ni wazima na unaona jinsi gani wapo kwenye kiwango kizuri, kutokana na uzoefu wao naamini watatusaidia kwenye mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Simba,” alisema Cheche.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.