


WAKAZI wa Kitongoji Cha Razaba Wilayani Bagamoyo Wameelezea masikitiko yao juu ya kufutwa kwa kitongoji hicho na uongozi wa serikali ya Wilaya jambo linalodaiwa kuwanyima haki ya kujiandikisha na kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.
Global TV Online imefika eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wawakilishi wa wananchi na viongozi wa ngazi za kijiji ambao walielezea masikitiko yao na kumwomba Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuingilia kati ili kuwanusuru na janga la kukosa makazi linalowakabili.
Wakazi hao walisema kuwa, wamezaa watoto na baadhi yao tayari walikwisha oa na kuolewa wakiwa eneo hilo hivyo wanashangaa kupatiwa taarifa ya mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kuwataka kuondoka pasipokujua waende wapi. Kilio chao wakakielekeza kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili aweze kutatua mgogoro uliopo kwenye eneo hilo, licha yao wao kudai kwamba kama ni eneo la serikali basi waoneshwe eno lingine la kwenda.
Aidha, Global TV Online kutaka kujua ukweli wa madai hayo ulizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa ambaye alifunguka haya.