The House of Favourite Newspapers

Wadau Wa Internet Wapigwa Msasa

0
 Meneja wa Kanda ya Afrika, Bwana Victor Ndonnang kutoka nchini Nigeria (kulia) akiwapa somo wanaliohudhuria.

Wadau na wanachama wa chama cha Internet Societ (ISOC) wamepigwa msasa na Meneja wa Kanda ya Afrika, Bwana Victor Ndonnang kutoka nchini Nigeria.

Mkutano huo ulifanyika Chuo Kikuu Huria Kinondoni Dar ambapo Nannang aliwafundisha wanachama hao mambo mbalimbali kuhusu matumizi bora na sahihi ya Internet ikiwemo faida na hasara zake.

Rais wa Chama cha Internet Society hapa nchini, Nazar Nicholas akizungumza na wanahabari.

Nannang aliwaeleza wadau hao changamoto za Internet zilizopo nchini Nigeria na kujionea changamoto  za hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari Rais wa Chama cha Internet Society hapa nchini, Nazar Nicholas amesema wanamshukuru Nannang kwa somo alilotoa.

Nazar amesema watu wengi wakiwemo vijana wamekuwa wakiutumia vibaya mtandao wa Internet na kujikuta wakiishia pabaya.

Rais huyo aliwashauri watu mbalimbali kuitumia Internet kwa ajili ya kujipatia maendeleo na kujitafutia majanga.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

Leave A Reply