×

MUTRAH: Hata Iweje, Sivai Nguo ya Milioni!

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii nzuri ya My Style, kama ilivyo ada hapa huwa tunakuletea mastaa mbalimbali Bongo ambao wanaelezea maisha yao ya kila siku nje ya sanaa.

 

Leo tunaye msanii wa Bongo Muvi, Mutrah Tamim ‘Mutra’ ambaye amezidi kupata umaarufu baada ya kuchaguliwa kuwa Mtanzania pekee kuigiza Tamthiliya ya Pete huko nchini Kenya ambayo inarushwa katika Chaneli ya Maisha Magic Bongo.

Msanii huyu mpaka sasa ameshacheza muvi kadhaa ikiwa Wake Up na Sikitu. Ungana nami katika My Style:

 

My Style: Ratiba yako kwa siku ukiamka ikoje?

Mutrah: Ratiba yangu siku hizi imebadilika kutokana na mtoto. Siku hizi nawahi sana kuamka kisha baada ya hapo nitacheza na mwanangu, nitakunywa chai na mwisho nitaondoka kwenda kwenye mihangaiko yangu ya kila siku.

 

My Style: Ukiwa na msongo wa mawazo ni sehemu gani hapa mjini ambayo unapenda kutembelea?

Mutrah: Inategemea na aina ya mawazo niliyonayo, kama yamenizidi uwezo basi huwa namkimbilia Mungu yaani nitaenda Msikitini, nitaswali sana na kumtolea Mungu sadaka basi nikitoka hapo nakuwa mwepesi.

Kama ni mawazo ya kawaida tu basi huwa natafuta sehemu iliyotulia vizuri kama vile ufukweni, napaki gari yangu pembeni kisha natulia natafakari jambo la kufanya.

My Style: Starehe yako kubwa ni nini?

Mutrah: Starehe yangu kubwa ni kuwa karibu na familia yangu basi.

My Style: Siku ukiamua kuvunja kabati juu mpaka chini huwa unatumia kiasi gani cha pesa?

Mutrah: Mara nyingi mimi huwa napenda kuwa simpo, hivyo huwa situmii gharama kubwa sana kwenye mavazi. Nguo hizohizo nilizonazo ndio ikitokea shughuli naenda nazo lakini ninachokifanya mimi ni kubadilisha tu kama kipindi hiki nilivaa hivi basi kipindi kingine nitavaa vingine.

 

My Style: Kiasi gani cha pesa huwezi kutoa kununua nguo hata iwe nzuri vipi?

Mutrah: Siwezi kutoa shilingi milioni 1 kununua nguo.

My Style: Sehemu gani ya mwili wako unaipenda sana?

 

Mutrah: Sehemu zangu za siri.

My Style: Wewe ni chizi nini hasa?

Mutrah: Mimi nina ugonjwa wa kupenda saa, naweza kusema ni chizi saa.

My Style: Msanii gani hapa Bongo mapigo yake yanakuvutia?

 

Mutrah: Wapo wengi sana siwezi kumtaja mmoja maana itakuwa ni upendeleo

My Style: Unatumia gari ya aina gani na gari ipi ni ya ndoto yako?

Mutah: Natumia Toyota Crown, gari ya ndoto yangu ni BMW.

My Style: Unapenda rangi gani za nguo?

Mutrah: Napenda sana rangi nyeusi.

 

My Style: Aina gani ya nguo ukivaa unaona unapendeza zaidi?

Mutrah: Napenda kuvaa jinz na tisheti ambazo zinashika vizuri kifua changu, kwa sababu ndio huwa naona napendeza zaidi kuliko nikivaa nguo za aina nyingine.

My Style: Unapenda kumuona mke wako akiwa katika muonekano upi wa mavazi?

Mutrah: Nikitoka naye mara nyingi huwa napenda avae mavazi ya kidini sana, lakini nikiwa naye nyumbani huwa napenda avae mavazi flani hivi… nadhani wakubwa wamenielewa, yaani nguo laini laini hivi.

 

My Style: Unaweza kutoka naye akiwa hana ‘make up’ usoni?

Mutrah: Huwezi amini, ndio napenda hivyo kutoka naye akiwa hajapaka make up, kuliko akiwa amepaka maana ndio namuona mzuri zaidi.

My Style: Una mbunifu wa mavazi pindi unatoka kwenda kwenye shughuli au huwa unabuni mwenyewe?

 

Mutrah: Mara nyingi huwa najivalisha mwenyewe, labda mara chache meneja wangu Lamata ndio kuna muda huwa ananishauri kwamba vaa hivi vaa vile na mke wangu pia.

My Style: Unapendelea chakula gani.

Mutrah: Ndizi za kukaanga, kachumbari pamoja na soseji.

My Style: Asante sana Mutrah.

Mutrah: Karibu tena!

MAKALA: Memorise Richard

Leave a Comment