BABA wa msanii wa vichekesho mtandaoni, Anko Zumo analipwa kutokana na kazi kubwa ya kumkaririsha maneno ya kuigiza mwanaye Mai Zumo (5).
Akipiga stori na Over Ze Weekend, Anko Zumo alisema amekuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha anamkaririsha mwanaye maneno ambayo anatakiwa kuyazungumza kwenye sini zozote ambazo huwa anacheza.
“Nalipwa kutokana na kumfundisha Mai, akipewa sini kwa kuwa ni mdogo huwa anachukulia kama michezo tu ya kitoto, kwa hiyo huwa nakaa naye namwambia tamka kitu fulani anatamka, namkaririsha na siku ya kushoot ikifika nakuwa bado namkumbusha yale maneno,” alisema Anko Zumo.
STORI: NEEMA ADRIAN