×

Mwonekano Mpya wa Kanye West Gumzo

RAPA maarufu na nguli kutoka nchini Marekani, Kanye West ametengeneza headlines nyingine tena kama kawaida yake ya kufanya vitu visivyokuwa vya kawaida na kuacha mijadala miongoni mwa mashabiki zake na mitandao ya kijamii.

Kanye ambaye haishiwi vibwanga ameamua kupafomu huku akiwa amejipaka na kuvaa mavazi rangi ya fedha (silver) kuanzia kichwani hadi miguuni.

Rapa huyo anayemiliki kanisa, alitokelezea katika muonekanao wa silver yeye pamoja na kwaya yake walipopafomu katika tamasha la Art Basel lililofanyika uwanja wa Marine, Miami, juzi Jumapili, Desemba 8, 2019.

Hata hivyo, Kanye aliibua maswali yasiyokuwa na majibu kuhusu ni kwa nini ameamua kuweka mwili wake kwenye muonekano huo.

 

 

Leave a Comment