
Na Hamida Hassan
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan anatia huruma baada ya kuibuka na kusema kuwa unene unaomuandama unamnyima raha kwani kila kukicha anazidi kuongezeka.
Akizungumza na Ijumaa Tiko alisema kuwa, watu wengi wakimuona wanamshangaa mpaka anajisikia vibaya lakini hana njia ya kufanya ili ajipunguze kwani ameshahangaika kwenye majumba yote ya mazoezi ‘gym’ lakini hajafanikiwa.
“Mimi hapa najiona nimepungua kidogo lakini nashangaa nikikutana na watu wananishangaa bado, najikuta nakata tamaa, kusema ukweli hata sijui nini kitanifanya nipungue, nachanganyikiwa mwenzenu,” alisema Tiko.