×

Mama wa Mwandishi Kabendera Amwangukia JPM

VERDIANA Mjwahuzi (81), mama wa mwandishi wa habari za kiuchunguzi, Erick Kabendera,  amemwomba  amsamehe mwanaye wa pekee anayemsaidia katika matibabu.

 

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh. milioni 173 na tayari amemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka kukiri makosa na kuomba msamaha.

 

Verdiana amesema, kati ya watoto wake wanane, Erick ni wa saba kuzaliwa na ndiye alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza lakini sasa ni maisha magumu hata dawa hapati.

 


Amesema, “Mheshimiwa Rais yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma, anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake.”

 


Ameongeza, “Kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda.”

 


Amesisitiza, “Nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.”

 

 

Leave a Comment