×

Trump Awashambulia Waliopiga Kura ya Kumwondoa Madarakani

 

MUDA mfupi baada ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kupitisha uamuzi wa kumshitaki Rais Donald Trump, mwenyewe ameitisha mkutano wa hadhara kuwashambulia vikali wajumbe wa Democrat waliopiga kura hiyo.

 

Baraza la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na wajumbe wa Democrat lilipiga kura hapo jana (Novemba 18) inayoidhinisha kushitakiwa kwa Trump kwa mashitaka matatu: kutumia vibaya madaraka, kulizuwia bunge kufanya kazi zake na kuhatarisha usalama wa nchi.

 

Wajumbe 230 waliidhinisha mashitaka hayo dhidi ya 197 waliopinga na kumfanya rais huyo wa 45 wa Marekani kuwa wa tatu kwenye taifa hilo kushitakiwa akiwa madarakani.

 

Muda mfupi baada ya uamuzi huo, Spika Nancy Pelosi ametuma ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akimuambia Trump kwamba hakuna aliye juu ya sheria. Mwakilishi wa Michigan kwenye Baraza hilo la Wawakilishi, Daniel Kildee, aliita jana kuwa siku ya huzuni lakini muhimu.

 

“Ninasikitika kwa sababu nyingi lakini pia nimeridhika kujua kwamba kwenye nchi hii unaweza kumwajibisha mtu yeyote aliyechaguliwa kupitia katiba. Hakuna anayefurahia hili, lakini inapendeza kuona kwamba Katiba yetu inafanya kazi,” alisema Kildee.

Leave a Comment