×

Niva: Unajizawadia Gari Bethidei Yako? Ukimtangazia Ndoa Umempata! – Video

 

MUIGIZAJI wa filamu za Bongo Movies, Niva Super Marioo,  amewaponda mastaa wanaojifanya wana pesa kumbe maisha yao ni ya kuungaunga tu.

 

Ametoa kauli hiyo wakati akipiga stori na Global TV Online kuhusu kazi zake za sanaa; “Sipendi tabia ya baadhi ya mastaa, eti anakodi gari halafu analileta kwenye bethdei yake, anajigea zawadi mwenyewe halafu analia kabisa, na mwisho wa siku hatumuoni nalo tena.

 

“Wasanii wanapenda sana kujikweza kama wana mkwanja lakini kiuhalisia ukikutana naye anakupiga mzinga, anakuomba hata shiulingi elfu kumi.  Sasa unajiuliza huyu huwa anatamba maisha yake ni mazuri, anakosa buku kumi kweli? Tuache maisha ya kuigiza.

 

“Mimi naweza kusema tu kwamba, kwa mwaka huu wa 2019, nimetimiza malengo yangu kwa asilimia 60, hakuna msanii wa filamu aliye bora kwa sababu hakuna aliyetoa muvi hata moja. Sio Ray, JB, mimi hapa, Aunt, Wema ama msanii mwingine yeyote. Nitashangaa kama zitatoka tuzo za msanii bora wa mwaka 2019, kwa kazi ipi? Mimi nitahoji,” amesema.

 

Ameongeza kwamba ameachia muvi yake mpya iitwayo Pigo la Nafsi, ambayo ipo kwenye application ya Sawhiliflix, kupitia simu za android na iOS.

 

“Ndani ya muvi hii yumo mdogo wangu, Hemmed PHD, na wasanii wengine kibao.  Kisa cha muvi hii kinaeleza namna ambavyo wanawake wa siku hizi ukiwatangazia ndoa hawachomoi, anakuja fasta, lakini vijana nao sasa akipata anachokitaka tu anatimua.  Hivyo wasichana waache kudanganyika,” alisisitiza.

 

Aidha,  ameeleza kuwa yupo mbioni kuachia muvi nyingine inayoitwa Presha ya Mke; “Movie iko poa sana, mimi sishindani na mtu, mtashindana na mimi. Mjiandae kuvaa pampasi za wakubwa. Kisa cha muvi hii ni kwamba, mke wangu ana majini mimi sina, nikitoka kuchepuka majini yake yanapanda lakini akichepuka yeye majini hayapandi.  Balaa linaanzia hapo,” alisema.

 

TAZAMA ALICHOKISEMA NIVA

Leave a Comment