×

Naibu Waziri Mgumba Amaliza Ziara Ya Siku Mbili Uganda

Naibu waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Omary Mgumba (kushoto) akiwa na Waziri Wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda Mhe Sempija.

Mhe Naibu waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Omary Mgumba amemaliza ziara ya siku mbili ya kiserikali nchini Uganda kwa kukutana na Waziri Wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda Mhe Sempija ambapo wamebadilishana uzoefu namna bora ya kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo hususani zao la kahawa katika nchi hizo mbili.

 

Katika mkutano wao walijadiliana kwa kina kuhusu utelekezaji wa makubiliano wa ushirikiano wa nchi zetu mbili kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa Septemba mwaka huu  Der es Salaam mbele ya marais wa nchi zote.

Miongoni mwa mashirikiano hayo ni pamoja na kubadilishana uzoefu, ujuzi na teknolojia za kuendeleza sekta ya kiliko mazao, ufugaji na uvuvi. Katika Kilimo mazao mkazo waliweka katika ushirikiano wa kilimo cha korosho, kahawa, mbegu za mafuta hususani michikichi na alizeti pamoja na kilimo cha miwa na viwanda vya sukari.

 

Vilevile waliongelea kuhusu kushirikiana namna ya kukabiliana kwa pamoja changamoto za kukabiliana na kilimo na biashara za mazao ya kilimo, mfumo wa masoko na sera za sekta ya kilimo hususani kahawa hasa kutokana na changamoto ya kuyumba na kushuka kwa bei ya zao hilo katika Soko la Kimataifa kutokana na kuongezeka kwa uzalisha kwa zaidi ya 65% kwa miongo miwili iliyopita kusikoendana na kasi, kuongezeka kwa wanywaji na watumiaji wa bidhaa za kahawa Duniani na kutegemea zaidi soko la nje kwa kahawa zikiwa hazijaongezewa thamani.

Pamoja na mambo mengine walijadiliana mikakati ya kuhamasisha unywaji wa kahawa katika mataifa yao, ukanda wa Afrika Masharini na Afrika kwa ujumla ili kutengeneza soko la ndani na kikanda kwa ajili ya kupunguza utegemezi wa soko la nje zaidi na kuinua soko kwa ujumla.

 

Mwisho walisisitiza wataalamu wa nchi zote mbili kukutana haraka iwezekanavyo ili kutengeneza mpango mkakati wa utekelezaji wa makubaliano ya mashirikiano ya kibiashara na uchumi katika sekta ya kilimo ili kuanza utekelezaji wa haraka kwa faida ya nchi zote mbili na watu wake. Sambamba na hilo pia Mhe. Mgumba alikutana na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo pamoja na wakulima na wawekezaji katika sekta ya kiliko nchini Uganda.

 

Mhe Naibu waziri Mgumba anarudi leo nchini baada ya kumaliza  ziara hiyo ya siku mbili nchi Uganda. Kabla ya ziara Hiyo Mhe Mgumba Alikuwa nchini Uganda katika Majukum ya kuliwakisha Bunge la Tanzanja na taifa kwa ujumla katika michezo ya Mabunge ya Afrika Mashari yaliyoanza Desemaba 8 hadi 18  nchini Uganda akiwa Mchezaji na Nahodha msaidizi wa timu ya mpira wa Miguu ya Bunge Sport Club.

 

Timu ya Bunge ya mpira wa miguuu ilifanikiwa kushika nafasi ya pili nyuma ya timu mwenyeji Bunge la Uganda iliyonyakua ubingwa wa mashindano hayo.

 

Timu ya Bunge ilirudi nyumba Desemba 2o huku  mashindano hayo yakitimiza matakwa ya masharti ya Jumuiya ya Afrika mashariki ili kujenga umoja, mshikamona na upendo miongoni mwa jumuiya hizo.

 

Mashindano hayo mwakani yatafanyika nchini kwa wenyeji wa Bunge la Jumuiya ya Africa Mashariki EALA ambapo makao makuu ni Arusha Tanzanaia. Mashindano yatafanyika Arusha Desemba 2020 muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.

Leave a Comment