×

Video Imeshtua Wengi, Baba Ataka Kumuua Mwanaye Mtoni

 

VIDEO liyosambaa katika mitandao ya kijamii jana Ijumaa, Desemba 20, 2019, jioni imeshtua watu wengi na kuzua taharuki huku wengi wao wakiwa na shauku ya kutaka kujua tukio hilo limetokea wapi na ilikuwaje.

 

Katika video hiyo, anaonekana mwanamme mmoja ambaye jina lake halijafahamika, anayedaiwa kuwa baba wa mtoto mwenye miaka kati ya 5 na 10, wote wakiwa watupu. Video inaonyesha wakiwa eneo la Maporomoko ya Maji ya Nguzi Camp.

 

Tukio hilo lililotokea Desemba 19, 2019, baba huyo akiwa na panga, alitaka kumdhuru (aidha kumuua ama kumjeruhi) mtoto huyo ndani ya maporomoko hayo.

 

Inadaiwa wasamaria wema walimshuhudia baba huyo akiwa katika mto huo na kupiga simu katika kituo cha polisi kilichokuwa karibu, ambao nao walifika haraka na kupambana na jamaa huyo wakijitosa majini na kumshambulia kwa kipigo hadi kumuokoa mtoto huyo akiwa hai.

 

 

Baada kupata taarifa kuwa tukio limetokea mkoani Morogoro, Global TV Online ilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Hamis Issah, lakini hakupatikana na alipotafutwa msaidizi wake, alikiri kupokea taarifa za tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi na leo Jumamosi, taarifa rasmi itatolewa.

 

ENDELEA KUFUATILIA GLOBAL TV ONLINE.

 

TAZAMA TUKIO ZIMA

Leave a Comment