
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa nyumba ya msanii na mtangazaji Mwijaku imezungushiwa utepe zimeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi.
Kufuatia taarifa hizo, Global TV imefika katika eneo la tukio ili kujionea hali halisi na kufanya mazungumzo na wakazi pamoja na watu mbalimbali waliokuwepo eneo hilo.
Kupitia mahojiano hayo, Global TV imekusanya maoni na taarifa kutoka kwa mashuhuda ili kubaini ukweli wa kilichotokea, huku ikifuatilia kwa karibu chanzo na sababu za tukio hilo lililozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.