
BAADHI ya wasanii wa tasnia mbalimbali nchini zikiwemo Bongo Fleva na Bongo Movies, wameungana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, kutembelea Mapango ya Amboni yaliyoko mkoani Tanga, kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania.
Wakizungumza na Global TV Online iliyoambatana nao kwenye ziara hiyo ya takribani siku tatu mkoani humo, wasanii hao wameeleza walivyojionea mengi yanayohusu utajiri wa asili wa Tanzania na kuahidi kuyatangaza kote duniani.