POLISI Mkoani Morogoro wanamshikilia Benson Bernard Sadala Shila (31) mkazi wa Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ambaye ni fundi Welding baada ya kukutwa uchi mtoni na mtoto wake aitwaye Goodchance Bernard (7), ambaye anasoma darasa la awali katika Shule ya Ebeneza mjini humo, huku akiwa na panga na msumeno akitaka kumdhuru mtoto huyo.